UN yalaani hukumu ya miaka 15 ya mwandishi Libya
3 Agosti 2020Matangazo
Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter Umoja wa Mataifa umesema hukumu hiyo inakiuka sheria za Libya pamoja na jukumu lake la kimataifa la kutoa maamuzi ya haki na uhuru wa kujieleza.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Libya Alan Bugeja amesema ana wasiwasi mkubwa hasa kutokana na hukumu hiyo hasa kwa kuwa mwandishi huyo alikuwa kizuizini kwa zaidi ya miaka miwili.
Uongozi mashariki mwa Libya haujaweka wazi hasa mashtaka yaliyokuwa yanamkabili mwandishi huyo, ila vyombo vya habari nchini humo vinasema alituhumiwa kwa kuwasiliana na mashirika yaliyopigwa marufuku katika eneo hilo la Libya.