1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yalaani kuhusu ukatili katika vita nchini Sudan

10 Februari 2026

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema ukatili uliotekelezwa katika mji wa El-Fasher wa Sudan mwezi Oktoba mwaka uliopita ungeliweza kuzuilika.


Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker TurkPicha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/picture alliance

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema ukatili uliotekelezwa katika mji wa El-Fasher wa Sudan mwezi Oktoba mwaka uliopita ungeliweza kuzuilika na kuonya kwamba sasa kuna hatari ya kurudiwa kwa ukatili kama huo huko Kordofan ambako mapingano yameongezeka katika siku za hivi karibuni.

Mkuu huyo ameyasema hayo wakati akitoa taarifa mpya kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu hali huko El-Fasher,ambapo amelaani matukio hayo ya kutisha baada ya kikosi cha  wanamgambo wa RSF kuanzisha "wimbi la mashambulizi makali  na kuuzingira kikatili mji huo kwa miezi 18.

Vikosi vya Sudan vimekuwa vitani na wanamgambo wa RSF tangu Aprili 2023. Mzozo huo umeua maelfu ya watu, na kuwafanya mamilioni wengine kukosa makazi na kusababisha kuwa mojawapo ya migogoro mibaya zaidi ya kibinadamu duniani.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW