1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yalaani unyanyasaji dhidi ya wafanyakazi wa kiutu

19 Agosti 2024

Umoja wa Mataifa umelaani kiwango kisichokubalika cha unyanyasaji na vurugu dhidi ya wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu.

Wafanyakazi 280 wanaotoa misaada ya kiutu waliuawa katika jumla ya mataifa 33 mnamo mwaka 2023.
Wafanyakazi 280 wanaotoa misaada ya kiutu waliuawa katika jumla ya mataifa 33 mnamo mwaka 2023.Picha: Loey Felipe/UN Photo/Xinhua/picture alliance

Kulingana na Umoja wa Mataifa, wafanyakazi 280 kati yao waliuawa katika jumla ya mataifa 33 mnamo mwaka 2023.

Umoja huo umeonya kwamba vitendo hivyo vimekuwa vikishuhudiwa mara kwa mara na vita vya Israel na Hamas huko Gaza vinaweza kusababisha idadi kubwa zaidi ya vifo hivyo mwaka huu.

Joyce Msuya, kaimu mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA), amesema katika taarifa yake siku ya Jumatatu, ikiwa dunia inaadhimisha Siku ya Huduma za Kibinadamu Duniani kuwa kuhalalisha unyanyasaji dhidi ya wafanyakazi wa kutoa misaada na ukosefu wa uwajibikaji havikubaliki na vina madhara makubwa kwa shughuli za misaada kote duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW