UN yaongeza muda wa vikwazo vya silaha nchini Sudan Kusini
31 Mei 2024Azimio lililowasilishwa na Marekani, lilipitishwa kwa uungwaji mkono wa kiwango cha chini zaidi kilichohitajika, huku nchi tisa zikiunga mkono na sita zikikosa kushiriki kura hiyo.
Azimio lashtumu kuongezeka kwa vurugu Sudan Kusini
Azimio hilo lilishtumu kuendelea kuongezeka kwa ghasia, ikiwa ni pamoja na vurugu kati ya jamii, na kurefusha mgogoro wa kisiasa, usalama, kiuchumi na kibinadamu katika maeneo mengi ya nchi hiyo.
Soma pia:Uhalifu mpya wa kivita waripotiwa Sudan Kusini
Azimio hilo linaongeza muda wa vikwazo vya silaha kwa nchi hiyo kwa mwaka mmoja hadi Mei 31, 2025.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Robert Wood, amesema vikwazo hivyo bado ni muhimu katika kuzuia mtiririko wa silaha katika eneo hilo lililojaa bunduki.
Sudan Kusini yapinga kuongezewa vikwazo
Serikali ya Sudan Kusini imepinga msimamo huo, pamoja na nchi kadhaa wanachama wa Baraza hilo la Usalama zinazoijumuisha Urusi, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitaka kuondolewa kwa vikwazo hivyo.