1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaonya kuhusu mashambulizi ya kulipiza kisasi Sudan

16 Januari 2025

Umoja wa Mataifa umesema ripoti kuhusu machafuko katika eneo la Al-Jazira zinazusha hofu kubwa kuhusu ukiukaji wa wazi wa sheria ya kimataifa.

Omdurman Sudan 2024 |  Machafuko yanayoendelea
Mashirika ya haki yameripoti kuwa wapiganaji wanaoliunga mkono jeshi wanafanya mashambulizi kwa misingi ya kikabila dhidi ya jamii za walio wachache kwenye jimbo hilo linalojishughulisha zaidi na kilimo.Picha: Amaury Falt-Brown/AFP

Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu mashambulizi ya kulipiza dhidi ya raia katika jimbo la Al-Jazira nchini Sudan.

Umesema ripoti za machafuko katika eneo hilo zinazusha hofu kubwa kuhusu ukiukaji wa wazi wa sheria ya kimataifa.

Jeshi la Sudan, ambalo lipo vitani na wanamgambo wa RSF tangu Aprili 2023, limefanya mashambulizi kwenye jimbo hilo wiki hii, na kuukomboa mji mkuu Wad Madani.

Mashirika ya haki yameripoti kuwa wapiganaji wanaoliunga mkono jeshi wanafanya mashambulizi kwa misingi ya kikabila dhidi ya jamii za walio wachache kwenye jimbo hilo linalojishughulisha zaidi na kilimo.

Watu 13 wameripotiwa kuuawa wakiwemo watoto wawili. Mratibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinaadamu nchini Sudan, Clementine Nkweta-Salami anasema "kulipiza kisasi na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia na vitu vya kiraia vimepigwa marufuku na sheria ya kimataifa ya kibinadamu".

Mashirika ya haki katika eneo hilo yanaripoti kuwa jamii za Kanabi -- wakazi wa mitaa ya mabanda na wanafanyakazi wa shughuli za kilimo kutoka maeneo mengine ya Sudan, zinatuhumiwa kwa kushirikiana na wanamgambo wa RSF, waliodhibiti jimbo la Al-Jazira kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW