UN yaonya watu wengi zaidi wataangamia Gaza
27 Oktoba 2023Hii ni baada ya karibu wiki tatu za mashambulizi ya Israel ya kulipiza shambulizi kali kabisa la Hamas kuwahi kufanywa katika historia ya nchi hiyo.
Umoja wa Mataifa aidha umeibua wasiwasi kuhusu kile ilichokiita uhalifu wa kivita unaofanywa wakati mzozo mkali wa Israel na Hamas ukiingia siku ya 21.
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwashughulikia Wakimbizi wa Kipalestina - UNRWA, Philippe Lazzarini amesema watu katika Ukanda wa Gaza wanakufa, na sio kutokana na mabomu pekee, bali wengi watakufa kutokana na matokeo ya mzingiro uliowekwa na Israel
Soma pia:UN: Israel na Hamas wanatenda uhalifu wa kivita
Jeshi la Israel limesema askari wake walifanya uvamizi mwingine wa muda mfupi wa ardhini ndani ya Gaza wakati likijiandaa kwa mashambulizi kamili ya ardhini.