1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

UN yapitisha azimio kupeleka misaada Syria

Zainab Aziz Mhariri: Josephat Charo
10 Januari 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kuunga mkono azimio la kuwepo wazi mpaka kati ya Uturuki na Syria kwa ajili ya kupeleka misaada kwenye eneo la kaskazini-magharinbi mwa Syria linaloshikiliwa na waasi.

USA Sicherheitsrat der Vereinten Nationen
Picha: Mike Segar/REUTERSS

Kuidhinishwa kwa azimio hilo sasa kutaruhusu kupelekwa misaada nchini Syria kutoka upande wa Uturuki kupitia kivuko cha Bab al-Hawa bila kuhitaji idhini ya serikali ya Syria.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema baada ya kura hiyo kwamba kwa kupitia mipakani ili kifikisha misaada nchini Syria itabaki kuwa ni njia ya lazima kwa ajili ya watu wapatao milioni 4.1 wa kaskazini magharibi mwa Syria.

Guterres amesisitiza kwamba hatua hii imechukuliwa wakati ambapo mahitaji ya kibinadamu yameongezeka na kufikia katika viwango vya juu tangu kuanza mzozo nchini Syria mnamo mwaka 2011.

Mwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield amesema kura hiyo inawapa watu wa Syria fursa ya kupumua pumzi za furaha na ameongeza kusema kwamba ijapokuwa shughuli hiyo ya kuokoa maisha ya watuwa Syria itaendelea lakini mengi zaidi mengi zaidi bado yanayohitaji kufanyika.

Azimio hilo limepitishwa kwa wingi wa kura ambapo misaada sasa itaendelea kupelekwa kwenye eneo la kaskazini magharibi mwa Syria linaloshikiliwa na waasi kwa muda wa miezi sita ijayo.

misaada ya Umoja wa Mataifa kwa wahitajiPicha: OMAR HAJ KADOUR/AFP

Hata hivyo katika hatua ya kushangaza Urusi ambayo ni mshirika mkuu wa Syria imeunga mkono azimio hilo.

Soma:Azimio la UN la muda wa kutoa misaada Syria laleta hisia mseto

Macho yote yaliikodolea Urusi, ambayo mara kwa mara ilijiepusha au ilitumia kura yake ya turufu kupinga maazimio juu ya ufikishaji wa misaada nchini Syria.

Urusi:Hatua ya kutoa misaada ni ya muda

Tangu miaka ya mwanzo ya vita, Uturuki imekuwa inawaunga mkono waasi wa Syria. Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vassily Nebenzia amesema kuuunga mkono azimio hilo sio kwamba kuna mabadiliko kulingana na msimamo wa kanuni za Urusi kuhusu utoaji wa misaada inaoingia Syria kwa kuvuka mpaka ambayo ilianza tangu mwaka 2014.

Amesisitiza kwamba hatua hiyo ni ya muda na inapaswa kubadilishwa na serikali ya Syria iliyo na haki ya kudhibiti utoaji wa misaada nchini mwake.

Ukata wa maji Syria

01:20

This browser does not support the video element.

Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa Bassam Sabbagh kwa upande wake amezikosoa nchi za Magharibi kwa kuingiza siasa katika shughuli zinazohusu misaada ya kibinadamu, amesema vikwazo vya nchi za Magharibi vimezidisha mateso kwa raia wa Syria ingawa serikali imekuwa ikifanya kazi bila kuchoka kutoa huduma za msingi kwa Wasyria wote.

Chanzo:AP

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW