UN yarefusha muda wa kikosi chake cha amani huko Abyei
15 Novemba 2025
Matangazo
Wanachama 12 waliunga mkono azimio hilo huku Urusi, China na Pakistan zikikosa kushiriki. Azimio hilo la kuongeza muda kwa kikosi hicho cha kulinda amani kinachojulikana kama UNISFA lilitayarishwa na Marekani ili kuongeza muda wa ujumbe huo hadi Novemba 2026.
Linasema kuwa Baraza la Usalama lina "nia" ya kurefusha zaidi muda wa ujumbe huo haswa kwa kuunda jeshi la polisi la pamoja la Abyei na kumaliza kabisa shughuli za kijeshi kama ilivyokubaliwa na pande hizo mbili mnamo mwaka 2011.
Azimio hilo pia linamtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuwasilisha ripoti ifikapo Agosti 2026, kuhusu maendeleo yoyote yatakayofanywa na nchi hizo mbili na kutathmini kuhusu kitakachotokea ikiwa kikosi hicho kitapunguzwa.