1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaridhia azimio la kupinga chuki za kidini duniani

Hawa Bihoga
12 Julai 2023

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa leo limeidhinisha azimio linaloyahimiza mataifa duniani kuchukua hatua za kupambana na chuki za kidini zinazochochea ubaguzi lililowasilishwa na Pakistan.

UN Sondersitzung Sudan
Picha: FABRICE COFFRINI/AFP/Getty Images

Kwenye kikao cha baraza hilo kinachoendelea mjini Geneva, mataifa 28 yamepiga kura za ndiyo kuidhinisha azimio hilo huku nchi 12 zikilipinga na nyingine 7 zikijizuia kupiga kura.

Chini ya azimio hilo, mataifa ulimwenguni yanatolewa mwito wa kuzipitia upya sheria na kuziba mianya inayoweka vizingiti vya kushughulikiwa kwa matendo yanayochochea chuki za kidini.

Awali, mkuu wa shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Volker Türk, alitumia mjadala huo kuhoji mpaka baina ya uhuru wa kujieleza na kuheshimu imani za kidini na kutoa wito wake wa kuheshimu wengine wakiwemo wahamiaji, na wanawake na wasichana wanaovaa hijabu na wapenzi wa jinsia moja.

Soma pia:UN yahimiza hatua za kupambana na chuki za kidini

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Haki za Binaadamu mjini Geneva, Uswisi, Türk alikosoa chuki na ubaguzi vinavyochochea vurugu wakati kukiwa na wasiwasi kuhusu matukio ya kukosa kuvumiliana yakilenga kujenga mgawanyiko kati ya tamaduni mbalimbali duniani.

"Watu wanahitaji kutenda kwa heshimu wengine." Türk aliliambia baraza hilo mapema kabla ya zoezi la kupigia kura azimio hilo lililopata upinzani mkubwa kutoka nchi za Magharibi.

Alisema kuna umuhimu wa uweka kando kwa muda swali la kile ambacho sheriainasema kinaruhusiwa au la na bila kujali imani ya mtu binafsi ya kidini au ukosefu wa imani.

Marekani yaongoza kupinga azimio hilo

Hata hivyo, azimio hilo limepingwa vikalina mataifa mengi ya Magharibi yakiongozwa na Marekani yanayosema linatishia uhuru wa watu kujieleza.

Mkuu wa shirika la Haki za Binadamu Umoja wa Mataifa Volker TurkPicha: FABRICE COFFRINI/AFP/Getty Images

Marekani ilisema isingeuliunga mkono azimio hilo, ikidai kuna wasiwasi kwamba linaweza kukanyaga haki ya msingi ya uhuru wa kujieleza.

"Kwa kujaribu kupiga marufuku kujieleza kwa namna hiyo kunaweza kuchochea chuki zaidi."

Alisema Rashad Hussain, ni mjumbe maalum wa Marekani kuhusu uhuru wa kidini.

Matukio ya hivi karibuni ya uchomaji nakala za kitabu kitakatifu kwa Waislamu, Qur'an, yamekuwa na madhara makubwa na hata kuchochea msimamo wa Uturuki, taifa lenye idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu barani Ulaya, kushadidia uliokuwa msimami wake wa kupinga maombi ya Sweden kujiunga na  Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Mjadala huo wa Baraza la Haki za Binaadamu, ulijikita kwenye maadili ya mataifa ya Magharibi yanayolaani ukosefu wa kuvumiliana lakini yakisisitiza haki ya uhuru wa kujieleza.

Soma pia:Umoja wa Mataifa wajadili chuki dhidi ya Waislamu

Mataifa yalio na idadi kubwa ya Waislamu yanayozitaka serikali kuimarisha mifumo yao ya kisheria ili kupiga marufuku uhuru wa kujieleza uliochupa mipaka ya kuingilia imani za kidini na kuchochea chuki ambavyo vinaweza kusababisha vurugu, ubaguzi na uhasama:

Maafisa wa Pakistan na Palestina waliongoza msukumo wa azimio la baraza hilo la haki za binaadamu ambalo pamoja na mambo mengine lilizitaka nchi kuchukua hatua za "kuzuia na kushtakivitendo na utetezi wa chuki za kidini ambazo zinajumuisha uchochezi wa ubaguzi, uhasama au vurugu."

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW