UN yaridhia mkataba wa uhamiaji
10 Desemba 2018Pamoja na kuwepo kwa harakati zilizosababisha mataifa kadhaa kujiweka kando na makubaliano hayo, zinazoendeshwa na kundi lenye siasa kali lenye kupinga wahamiaji, lakini mkataba huo unasimamia usalama, mwenendo na udhibiti wa uhamiaji uliridhiwa. Jitihada za awali hatua hiii ya leo zilihitimishwa Julai 18 baada ya mazungumzo yaliodumu kwa miezi kadhaa.
Lakini Marekani na mataifa na mataifa mengine 30 yalijiondoa au kuonesha wasiwasi, ambapo mengine yalidai mkataba huo unakiuka uhuru wa ndani wa kitaifa. Kwa mujibu wa makubaliano hayo kila taifa lina haki ya kuzitolea ufafanuzi sera zao za uhamiaji na kutolea maelezo pia ukomo wao, lakini lazima watekeleze kwa kuzingatia matakwa ya haki za binaadamu ya kimataifa wakati wanayafanya hayo.
Malengo 23 ya mkataba wa uhamiaji
Mkataba huo,ambao haufungamanishwi kisheria na ambao unatazamwa kama makubaliano ya kwanza ya kimataifa kuhusu uhamiaji, unajikita katika malengo 23 ukiweka misingi ya kisheria kwenye uhamiaji na kufifisha matumizi ya uvukaji wa maeneo ya mipakani isiyo rasmi, katika kipindi hiki ambacho idadi ya watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine dunianio kote ikipindukia watu milioni 250.
Pedro Sanches, waziri Mkuu wa Uhispania alisema "Makubaliano ya kimataifa ambayo yameridhiwa leo hii mjini Marrakesh yanatufungulia njia kwetu sote, ya kuwa na namna sahihi itakayotupa uelekeo wa kushughulikia wimbi la uhamiaji. Kwa ushirikiano wa kimataifa utakaojikita katika mgawanyo wa majukumu na mshikamano wa kufanya kazi kwa pamoja, ninashawishika kwamba tutaweza kupata jawabu."
Nae katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteres ameielezea hatua hiyo, kama ramani ya kudhibiti mateso na vurugu. Kiongozi huyo ameyataka baadhi ya mataifa kuachana na imani potofu yakiwemo madai ya kwamba mkataba huo utatoa ridhaa ya Umoja wa Mataifa kuunda sera uhamiaji kwa matiafa wanachama.
Akizungumza mbele ya Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Rais wa Panama Juan Carlos Varela na Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras. Katibu Mkuu Guteres alisema lazima tuishinde hofu na tafsiri potofu. Mataifa 10 mengi ya hayo kutoka katika eneo lililojulikana kama la Kikomunisti, Ulaya Mashariki yamejiondoa.Mengine sita likiwemo la Israel na Buligaria bado yanatafakari yataunga mkono mkataba huo au yajitoe.
Mwandishi: Sudi Mnette RTR/AFP
Mhariri:Yusuf Saumu