UN yasema haina mabilioni ya dola kulisha wenye njaa duniani
18 Novemba 2025
Matangazo
Katika taarifa yake, shirika hilo limesema kupungua kwa ufadhili kwa huduma za kibinadamu duniani kunalilazimisha shirika hilo kutoa kipaumbele cha msaada wa chakula kwa takribani theluthi moja ya wale wanaohitaji na kuwalenga watu milioni 110 wanaokabiliwa na hatari zaidi.
WFP inahofia kiwango kidogo zaidi cha ufadhili
Pia limekadiria kwamba hatua hiyo italigharimu shirika hilo dola bilioni 13, lakini likaonya kuwa "makisio ya sasa ya ufadhili" yanaonyesha WFP inaweza kupokea nusu tu ya kiasi hicho.
WFP imesema watu milioni 318 wanaokabiliwa na njaa kali ni zaidi ya mara mbili ya idadi iliyorekodiwa mwaka 2019, huku mizozo, hali mbaya ya hewa na kuyumba kwa uchumi kukiwaathiri.