1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

UN yasema iko tayari kupeleka chakula katika eneo la Darfur

17 Agosti 2024

UN imesema iko tayari kuanza kupeleka chakula katika eneo lenye vita la Darfur Magharibi mwa Sudan, baada ya serikali ya nchi hiyo kuamua kufungua tena kivuko muhimu cha mpaka cha Adre kilichoko kati ya Sudan na Chad.

Watu watoroka mapigano katika eneo la Darfur magharibi mwa Sudan kupitia kivuko cha Adre mnamo Agosti 4, 2023
Watu watoroka mapigano katika eneo la Darfur magharibi mwa Sudan kupitia kivuko cha Adre Picha: Zohra Bensemra/REUTERS

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, lilipongeza hatua hiyo na kusema ni muhimu katika harakati za kuokoa maisha.

Kufunguliwa kivuko cha Adre kutawezesha msaada kufikishwa Darfur

Msemaji wa shirika hilo la WFP nchini Sudan Leni Kinzli, amewaambia jana waandishi habari mjini Nairobi kwamba kufunguliwa kwa kivuko hicho cha Adre, ambacho ni muhimu kwa usambazaji wa misaada ya kibinadamu, kutawezesha kufikishwa misaada katika jimbo la Darfur linalokumbwa na migogoro nchini Sudan, ambako baa la njaa lilithibitishwa wiki mbili tu zilizopita.

Soma pia:Waasi wa Chad waushambulia mji wa Adre unaopakana na Darfur

Kinzli ameongeza kuwa malori mawili yakiwa na takriban tani 6,000 za chakula kwa ajili ya watu wapatao 500,000 yalikuwa yakipakiwa, ili kupelekwa katika  maeneo ya Darfur, mara tu watakapopata kibali cha serikali.