1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yasema msaada usio na kikomo unahitajika Gaza

27 Oktoba 2023

Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa msaada usio na kikomo unahitajika Gaza ikiwa ni baada ya wiki tatu za mashambulizi ya Israel.

Kamishna mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina - UNRWA, Philippe Lazzarini.
Kamishna mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina - UNRWA, Philippe Lazzarini.Picha: Mostafa Alkharouf/Anadolu/picture alliance

Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa msaada usio na kikomo unahitajika Gaza ikiwa ni baada ya wiki tatu za mashambulizi ya Israel ya kulipiza mashambulizi ya Hamas mwezi huu ambayo yamechochea mgogoro wa kiutu katika ukanda huo unaozingirwa wa Kipalestina.

Kamishna mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina - UNRWA, Philippe Lazzarini, amesemamsaada wa kutosha unahitajika katika Ukanda wa Gaza, akisema msaada unaoingia kwa sasa ni kama makombo. 

Soma pia:UN yasema msaada usio na kikomo wahitajika Gaza

Lazzarini pia amethibitisha kuwa wafanyakazi 57 wa shirika hilo wameuawa katika vita hivyo.