1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMyanmar

UN yasema uhalifu wa kivita umeongezeka Myanmar

8 Agosti 2023

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema wamekusanya ushahidi wa kutosha juu ya kuongezeka kwa uhalifu wa kivita nchini Myanmar, ikiwa pamoja na mauaji ya halaiki na unyanyasaji wa kingono.

Myanmar | jeshi
Wanajeshi wa Myanmar wakifanya gwaridePicha: AFP/Getty Images

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema wamekusanya ushahidi wa kutosha juu ya kuongezeka kwa uhalifu wa kivita nchini Myanmar, ikiwa pamoja na mauaji ya halaiki na unyanyasaji wa kingono na wanajiandaa kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria.

Myanmar imekumbwa na ghasia za mauaji tangu kufanyika mapinduzi yaliyoiondoa serikali ya Aung San Suu Kyimnamo mwezi Februari mwaka 2021 na hivyo kuanzisha misako ya umwagikaji damu dhidi ya wapinzani na kusababisha mapigano kwenye maeneo mbalimbali ya nchini Myanmar.

Kitengo huru cha Umoja wa Mataifa kinachofanya uchunguzi juu ya Myanmar kimesema kinao ushahidi wa kuthibitisha kwamba wanajeshi wa nchi hiyo na wanamgambo washirika wanatenda uhalifu mkubwa wa kivita mara kwa mara.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa hawajaruhusiwa kwenda Myanmar lakini wameshirikiana na vyanzo zaidi ya 700 na wamekusanya taarifa zaidi ya milioni 23, hati, picha, video na ushahidi wa satelaiti juu ya Myanmar.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW