1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yasema watoto 7 wamekufa kwa baridi kali huko Gaza

6 Januari 2025

Shirika la misaada la Umoja wa Mataifa la Palestina limesema katika ripoti yake kwamba takriban watoto saba wamekufa kutokana na baridi kali na ukosefu wa makaazi huko Gaza.

Israel-Hamas Krieg | Israelische Angriffe auf Gaza | Al-Daraj
Watoto wa Kipalestina waliojeruhiwa katika Hospitali ya Baptist ya al-Ahli kwa matibabu kufuatia shambulio la Israeli kwenye Shule ya Musa bin Nasir, Gaza Desemba 22, 2024.Picha: Abdalrahman T. A. Abusalama/Anadolu/picture alliance

Kupitia mtandao wa X, Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesema kwamba watoto wachanga 7,700 katika eneo hilo lenye vita wanaishi katika makazi duni kutokana na mgogoro kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas. Mamlaka ya Israel inayohusika na masuala ya Palestina, COGAT,imesema kwenye mtandao wa X kwamba inafanya kazi na mashirika ya misaada ya kimataifa kama vile shirika la Rahma Worldwide ili kuwapa wakazi mahema, blanketi,nguo za joto na bidhaa za usafi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW