1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

UN yataka dola bilioni 4.2, msaada kwa Ukraine, 2024

15 Januari 2024

Umoja wa Mataifa umesema Jumatatu kuwa itahitaji dola bilioni 4.2 ili kutoa msaada wa kiutu nchini Ukraine katika mwaka wa 2024.

Mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths
Mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa Martin GriffithsPicha: Martial Trezzini/dpa/Keystone/picture alliance

Msaada huo ni pamoja na kuwasaidia mamilioni ya wakimbizi waliokimbia vita nchini humo.

Vita vya Urusi nchini Ukraine vinakaribia kuingia mwaka wake wa tatu ifikapo Februari.

Umoja wa Mataifa unatumai kuwafikia watu milioni 8.5 ndani ya Ukraine na wakimbizi milioni 2.3 na jamii zinazowahifadhi mashariki mwa Ulaya.

Taarifa ya Mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths inasema watu milioni 14.6 watahitaji msaada wa kibinaadamu nchini Ukraine mwaka huu -- ikiwa ni asilimia 40 ya jumla ya idadi ya watu.

Uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine Februari 2022 ndio uvamizi mkubwa kabisa wa nchi ya Ulaya tangu Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi unaolikumba bara hilo tangu mapigano hayo ya 1939 hadi 1945.