1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

UN yataka haki itendeke baada ya shule ya Iran kushambuliwa

27 Machi 2026

Umoja wa Mataifa umeitaka Marekani ikamilishe uchunguzi wake juu ya mauaji ya kutisha ya watoto 160 kwenye shule moja ya wasichana katika siku ya kwanza ya vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, mnamo Februari 28.

Münchner Sicherheitskonferenz 2026 |  Volker Türk,
Mkuu wa Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, Volker Turk,Picha: DW

Mkuu wa Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema kushambuliwa kwa shule hiyo ya msingi ya Shajareh Tayyebeh, kulibainisha ukatili usioelezeka dhidi ya watoto, na kwamba lazima kuwe na uwajibikaji kwa waliohusika.

Katika mkutano wa Baraza hilo mjini Geneva,  Turk alisema mvutano ulioko kwa sasa dhidi ya mataifa yaliyovitani, hauwezi kusuluhishwa kwa mauaji ya wanafunzi.

Amesema mauaji hayo yamefungua dirisha kubwa la hofu duniani na kwamba haki lazima itendeke.

Turk ameitolea mwito Marekani kukamilisha haraka uchunguzi wa shambulizi dhidi ya shule hiyo akisema matokeo yake ni lazima yatangazwe hadharani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW