1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatoa dola milioni 100 kukabiliana na matukio ya dharura

Angela Mdungu
31 Agosti 2024

Umoja wa Mataifa umetangaza kutoa dola milioni 100 zitakazotumika kukabiliana na matukio ya dharura ya kibinadamu katika nchi 10 za Afrika, Mashariki ya Kati, Asia na eneo la Carribean.

Kaimu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kiutu Joyce Msuya
Kaimu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kiutu Joyce Msuya Picha: Loey Felipe/UN Photo/Xinhua/picture alliance

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa msaada huo jana Ijumaa, Kaimu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kiutu Joyce Msuya amesema mataifa hayo yanakabiliwa na ukosefu wa fedha na kusababisha mashirika ya kiutu kushindwa kutoa msaada muhimu wa kuokoa maisha ya watu.

Zaidi ya theluthi moja ya ufadhili huo utaelekezwa Yemen na Ethiopia ambako watu wanakabiliwa na njaa, maradhi, majanga yanayotokana na hali ya hewa pamoja na changamoto ya watu kukosa makazi. Mataifa mengine yatakayopokea msaada huo ni pamoja na Myanmar, Mali, Burkina Faso, Haiti, Cameroon, Msumbiji, Malawi na Burundi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW