1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatoa wito kwa viongozi wa S. Kusini kuhusu uchaguzi

8 Novemba 2024

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa viongozi nchini Sudan Kusini kuonyesha dhamira yao juu ya mchakato wa mpito kuelekea demokrasia.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva KiirPicha: Andrew Burton/picture alliance/AP

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa viongozi nchini Sudan Kusini kuonyesha dhamira yao juu ya mchakato wa mpito kuelekea demokrasia, na kusisitiza kwamba muda unayoyoma wa kufanya mageuzi yanayohitajika kufuatia kucheleweshwa upya kwa maandalizi ya uchaguzi.

Balozi wa Umoja huo wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom, amesema hatua hiyo haiwezi kuepukika lakini ni hali yakusikitisha kwa raia wa nchi hiyo waliofadhaishwa na hali mbaya ya kisiasa na kutojitolea kwa viongozi wao kutekeleza makubaliano ya amani na pia kuleta mabadiliko ya kidemokrasia yaliyosubiriwa kwa muda mrefu.Sudan Kusini yaahirisha uchaguzi mkuu hadi 2026

Haysom ameongeza kuwa jamii ya kimataifa inahitaji ushahidi madhubuti kwamba viongozi wa nchi hiyo na vigogo wa kisiasa wamejitolea kwa dhati kwa mustakabali wa kidemokrasia.

Sudan Kusini, taifa changa zaidi duniani, ilitarajiwa kufanya uchaguzi wake wa kwanza tangu kujipatia uhuru wake mnamo mwezi Desemba,  lakini mwezi Septemba, Rais wa nchi hiyo Salva Kiir alitangaza kuwa uchaguzi huo hautafanyika hadi Desemba 2026.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW