UN yatoa wito wa mchango wa kukabiliana na nzige Afrika
11 Februari 2020Matangazo
Mark Lowcock amekiambia kikao cha wanahabari kuwa kuna watu milioni 13 katika nchi zilizoathirika ambao wanakabiliwa na kitisho kikubwa cha uhaba wa chakula sasa.
Watu milioni kumi kati yao wapo katika maeneo yaliyoathirika na nzige hao.
Lowcock ambaye amesema hivi karibuni alitoa kiasi cha dola milioni 10 kupambana na janga hilo, alionya kuwa kama hapatakuwa na suluhisho la haraka, kutakuwa na tatizo kubwa baadaye mwaka huu.
Nzige hao wameharibu vyakula nchini Kenya, Ethiopia na Somalia. Wameripotiwa kuvamia Uganda Jumapili.