1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatoa wito usitishwaji mapigano Pakistan na Afghanistan

25 Machi 2026

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa Afghanistan na Pakistan kukubaliana kwa mara nyengine tena kusitisha mapigano na kutafuta mkataba wa kudumu wa amani.

Afisa wa ulinzi wa Taliban akagua uharibifu wa shambulizi la Pakistan
Afisa wa ulinzi wa Taliban akagua uharibifu wa shambulizi la PakistanPicha: Wakil Kohsar/AFP

Hii ni baada ya kuzuka kwa ripoti za machafuko mapya ya mpakani Jumatano.

Afisa mmoja wa Afghanistan amesema vikosi vya Pakistan vimefanya mashambulizi 85 ya angani katika mkoa wa mashariki wa Kunar katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, ambapo maeneo ya makaazi ya watu yalishambuliwa.

Mashambulizi haya yanafanyika licha ya makubaliano ya muda mfupi ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa kwa ajili ya sherehe za sikukuu ya Eid. Pakistan haijatoa tamko lolote kuhusiana na mashambulizi hayo mapya.

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wanasema machafuko yaliyotokea mwishoni mwa mwezi Februari tayari yamesababisha vifo na majeruhi ya karibu watu 300 nchini Afghanistan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW