1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Vyama vya siasa fanyeni kampeni kwa uhuru Sudan Kusini

24 Novemba 2023

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini amehimiza vyama vyote vya kisiasa nchini humo viweze kufanya kampeni kwa uhuru wakati taifa hilo changa zaidi duniani likielekea kuandaa uchaguzi uliosubiriwa kwa muda mrefu.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva KiirPicha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Nicholas Haysom amesema haiwezekani kutarajia uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika Desemba 2024, ispokuwa vyama vyote vya siasa Sudan Kusini vitaweza kujiorodhesha na kufanya kampeni bila vitisho, na pia viongozi na wadau mbalimbali washirikiane kikamilifu ili kufikia hatua muhimu.

Uchaguzi huo utawezeshwa kutokana na mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2018 ambao ulipelekea pia kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mapema mwezi huu, Rais Salva Kiir, ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka 2011, alifanyia mabadiliko katika taasisi kadhaa za serikali zilizopewa jukumu la kusimamia uchaguzi huo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW