UN yazituhumu Urusi na Ukraine kwa kuwauwa wafungwa
25 Machi 2023![Gefangenenaustausch Russland Ukraine](https://static.dw.com/image/64913488_800.webp)
Tuhuma hizo zimetolewa baada ya Ukraine kudai kuwa wanajeshi wa Urusi walimuuwa mpiganaji wa Ukraine aliyechukuliwa video akisema "Utukufu kwa Ukraine" kabla ya kupigwa risasi.
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaofuatilia haki za binadamu nchini Ukraine Matilda Bogner, amesema shirika lake limerekodi mauaji kutoka pande zote mbili.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana Ijumaa, Bogner alisema wana hofu pia kuhusu taarifa za kuuwawa kwa wafungwa 25 wa Urusi uliofanywa na majeshi ya Ukraine.
Katika taarifa tofauti, wizara ya mambo ya kigeni ya Ukraine, iliushukuru Umoja wa Mataifa kwa kazi yao, lakini ilisisitiza kuwa inatarajia umoja huo utajiepusha na hatua zozote zinazoweza kutafsiriwa kuwa ni sawa na "kufananisha muathiriwa na mchokozi."