Migogoro
Wakimbizi 900 wa Rohingya wamekufa, hawajulikani waliko
17 Aprili 2026
Matangazo
Msemaji wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Babar Baloch amefafanua kuwa kati ya zaidi ya wakimbizi 6,500 waliojaribu kuvuka baharini, mmoja kati ya saba hajulikani aliko au alikufa maji. Amesema takwimu hizo zinaonesha idadi kubwa zaidi ya vifo kwa wakimbizi na wahamiaji wanaosafiri kwa njia ya bahari kote duniani.
Wengi wa wakimbizi wa Rohingya wanakimbia hali duni, unyanyasaji
Wakimbizi wengi wa Rohingya hutoka katika kambi kubwa za Cox's Bazar nchini Bangladesh, ambako zaidi ya milioni moja wanaishi katika hali duni. Wengi wao walikimbia kutoka jimbo la Rakhine la Myanmar ambalo linakabiliwa na mapigano kati ya jeshi na waasi wa Arakan. Huko, wamekuwa wakikabiliwa na unyanyasaji na kunyimwa uraia.