Migogoro
Zaidi ya wanawake, wasichana 38,000 waliuwawa vita vya Gaza
17 Aprili 2026
Matangazo
Idadi hiyo ni sawa na nusu ya idadi ya vifo 71,000 viivyotangazwa na Wizara ya Afya ya Msemaji wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa Sofia Calltorp amesema kando ya vifo hivyo, karibu wanawake na wasichana 11,000 walipata majeraha makubwa ambayo yamewafanya waishi na ulemavu maisha yao yote.
Ugumu wa maisha wazidi kuwaumiza wanawake
Calltorp ameongeza kuwa vita vimebadilisha maisha ya familia za Wapalestina ambapo maelfu ya wanawake ambao waume zao waliuwawa wanapambana kuziendesha familia bila kipato msaada wala huduma muhimu.