1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSomalia

UN: Zaidi ya Wasomali 140,000 wakimbia mafuriko

14 Aprili 2023

Zaidi ya watu 140,000 nchini Somalia ambako kunashuhudiwa ukame wamekimbia makaazi yao kufuatia mafuriko makubwa tangu katikati ya mwezi Marchi

Bildergalerie Mutterliebe
Picha: picture alliance/Photoshot

Takwimu hiyo imetolewa na ofisi ya  Umoja wa Mataifa inayoshughulikia migogoro,  ikionesha kwamba jumla ya watu 170,000 wameathirika na mafuriko huku mikoa ya Kusini ya Gedo na Bay yakiwa yameathirika zaidi.

Mafuriko hayo yametokana na msimu wa mvua ambao kwa kawaida huanza mwezi Machi na kundelea hadi mwezi Juni katika eneo hilo la upembe wa Afrika.

Hali ya hewa huenda ikasababisha matatizo zaidi ya hali ya kibinadamu. Hivi sasa Somalia inakabiliwa na maambukizi ya kipindupindu na maradhi mengine yanayoambukiza kupitia maji machafu.