UN: Zaidi ya watu 2,400 wamefariki Haiti
18 Agosti 2023Machafuko hayo yanatokana na magenge ya uhalifu. Haya ni kwa mujibu wa Shirika la Haki la Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa shirika hilo Ravina Shamdasani amesema leo kuwa, miongoni mwa hao waliouwawa ni watu 350 waliouwawa kwa kuchomwa na wakaazi na makundi ya kulinda usalama. Umoja wa Mataifa unasema pia kwamba watu 902 wamejeruhiwa kuanzia Januari mosi hadi Agosti 15. T
aarifa hii ya Umoja wa Mataifa inakuja baada ya kundi moja la kutetea haki za kibinadamu huko Haiti kusema kwamba watu 30 waliuwawa jana katika Mji Mkuu Port-au-Prince na dazeni nyengine ya watu kujeruhiwa.
Mtandao wa kitaifa wa kutetea haki za binadamu nchini Haiti umesema pia kuwa nyumba katika mtaa wa Carrefour zilichomwa moto katika mashambulizi hayo na maafisa wawili wa polisi wakauwawa pia.