1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Changamoto ya kupatikana muafaka wa kupunguza hewa ukaa

7 Desemba 2023

Watalaamu wa masuala ya hali ya hewa wamesema matokeo ya mazungumzo ya mazingira anayoendelea kwa miaka mingi yanaweza kukumbwa na utata kuhusu kukosekana muafaka katika kupunguza hewa ukaa inayoathiri mazingira.

UAE COP28 Klimakonferenz in Dubai
Francisco Vera, kutoka kushoto Emmanuel Jidisa, Lova Renee na Revan Ahmad wakiwa DubaiPicha: Rafiq Maqbool/AP Photo//picture-alliance

Watalaamu wa masuala ya hali ya hewa wamesema matokeo ya mazungumzo muhimu ya hali ya hewa yanayoendelea kwa miaka mingi yanaweza kukumbwa na utata kuhusu kukosekana muafaka kwenye kipengele kinachohusu namna ya kupunguza hewa ukaa inayoathiri mazingira. Lisa Fischer, mchambuzi wa jopo la E3G amesema huku ulimwengu ukipitia mwaka unaokabiliwa na joto kali, mioto na jamii zinazokumbana na mafuriko, wahusika katika mazungumzo ya COP28 lazima watoe majibu kulingana na tathmini ya Umoja wa Mataifa kwamba nchi bado ziko mbali mno kufikia malengo yao ya hali ya hewa. Rais wa COP28 Sultan Al Jaber, ambaye pia anaongoza kampuni ya taifa ya mafuta ya Umoja wa Falme za Kiarabu, ADNOC, amesema diplomasia ya hali ya hewa inapaswa kuzingatia kukomesha uzalishaji wa hewa ukaa na sio lazima mafuta.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW