1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Unafahamu nini juu ya mazungmzo ya kutafuta amani Ukraine?

26 Julai 2024

Meya wa mji mkuu wa Ukraine Kyiv Vitali Klitschko amewashangaza wafuatiliaji, kwa kuibuka na wazo la kuwepo makubaliano ya kimaeneo na Urusi.

Vitali Klitschko
Meya wa mji wa Kiev nchini Ukraine Vitali KlitschkoPicha: DW

Mjadala umeongezeka katika siku za karibuni kuhusu ikiwa vita vya Urusi nchini Ukraine vinaweza kumalizwa kwenye meza ya mazungumzo. Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban alimtembelea Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kile ambacho rais huyo wa zamani alikitaja kama "ujumbe wa amani."

Na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson hivi majuzi naye alidai katika andiko lake kwenye jarida la Daily Mail la Uingereza kwamba alimpa rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais wa sasa Donald Trump "mpango wa amani" ambao ungemhitaji Putin ajiondoe "angalau" kwenye mipaka aliyokamata kabla ya uvamizi wa 2022.

Ukraine yaashiria utayari wa kuzungumza na Urusi kuhusu vita

Urusi iliiteka Rasi ya Crimea nchini Ukraine kinyume cha sheria mwaka 2014 na tayari ilikuwa inadhibiti sehemu za mikoa ya Donetsk na Luhansk ya Ukraine hadi kufikia 2022. Kwa upande wake, Trump amejitanabahisha kwa nyakati tofauti, ikiwa ni pamoja na wakati wa kampeni za hivi karibuni, kwamba angevimaliza vita mara moja ikiwa atachaguliwa tena.

Lakini kilichowashangaza waangalizi wengi ni maoni ya Vitali Klitschko, meya wa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv kwamba Rais Volodymyr Zelenskyy anaweza kufikiria kuingia makubaliano ya kimaeneo na Urusi. Klischko alisema alipozungumza na gazeti la Italia la Corriere della Sera kwamba "Miezi michache ijayo itakuwa migumu sana kwa Volodymyr Zelenskyy.

"Je, aendeleze vita na vifo na uharibifu, au kuzingatia maelewano juu ya maeneo na Putin? Na katika suala kama hili, ni shinikizo gani litatoka Marekani ikiwa Trump atashinda?

China yajadili mipango ya amani na Ukraine

Klitschko aliongeza kuwa Zelenskyy "labda atalazimika kufanya kura ya maoni" katika suala hili. "Sidhani kama anaweza kufikia makubaliano machungu lakini pia muhimu peke yake na ambayo hayajahalalishwa na  umma.

Klitschko 'kutatua akaunti' na Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiwa na Meya wa mji wa Kiev Vitali KlitschkoPicha: ZUMA Press Wire/dpa/picture alliance

Je, kauli kama hizo kuhusu mipango ya amani na maelewano yanayoweza kutokea ya kimaeneo kwa upande wa Ukraine yanamaanisha kuwa nchi hiyo iko tayari kupata suluhu la kidiplomasia ili kumaliza vita? Je, hilo litakubaliwa na Waukraine na washirika wake wa Magharibi?

Volodymyr Fesenko, mkurugenzi wa Kituo cha Penta kinachotoa Mafunzo ya Kisiasa huko Kyiv, aliyataja maoni hayo ya Klitschko kama "mwanzo mbaya." Alisema hakuna mazungumzo ya kweli ya amani yanayofanyika kwa sasa, ila ni mipango tu ambayo hata haiweki msingi wa mazungumzo.

Alisema Klitschko alikuwa akijaribu kutengeneza mazingira mazuri na Zelenskyy, ambaye amekuwa akitofautiana naye kwa miaka mingi.

Podolyak: Makubaliano na Urusi ni kama 'makubaliano na shetani'

Lakini aliungana na Klischko kwamba suala kama hilo litatakiwa kuidhinishwa na Waukraine wote kupitia kura ya maoni, badala ya kumuachia Zelenskyy peke yake. Roger Hilton, mchambuzi wa taasisi ya kimataifa ya GLOBSEC, yenye makao yake katika mji mkuu wa Slovakia, Bratislava, alisema baadhi ya wanasiasa wa Ukraine wanaanza kuzungumzia makubaliano ya maeneo baada ya zaidi ya miaka miwili migumu sana ya vita.

Akasema "Na maoni haya ya meya yanaweza kuwa ni jaribio la ndani la kisiasa ili kuangalia ikiwa hata kama lingeweza kupokelewa na idadi ya watu."

Hilton aliongeza kuwa na si kwamba makubaliano ya ya kimaeneo yangekuwa machungu kwa Ukraine pekee, bali hata kwa mataifa mengine ya Ulaya. Kulingana na kura za maoni, Waukraine wanaotaka kufanya makubaliano ya kimaeneo wamekuwa wakiongezeka taratibu tangu msimu wa machipuko wa 2023, wakiamini itasaidia upatikanaji wa haraka wa amani.

Mnamo mwezi Mei, asilimia 32 ya waliohojiwa walisema wangekuwa tayari kufanya makubaliano, ikilinganishwa na karibu asilimia 10 ya Mei 2023. 

Mashambulizi ya Urusi yameua zaidi ya watu 30 Ukraine

02:10

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW