1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN:Bajeti ya 2020 juu, fedha za uchunguzi uhalifu wa kivita

Sekione Kitojo
28 Desemba 2019

Baraza kuu la Umoja wa mataifa liliidhinisha bajeti yake ya dola bilioni 3.07 ya kufanyia kazi ambayo kwa mara ya kwanza inajumuisha  fedha kwa ajili ya uchunguzi wa uhalifu wa kivita nchini Syria na Myanmar.

USA Narendra Modi Rede UN-Generalversammlung
Picha: Reuters/L. Jackson

Bajeti  hiyo inawakilisha  ongezeko  dogo kutoka  idadi  ya  mwaka 2019 ya  dola bilioni 2.9. Ongezeko  hilo  ni  kutokana  na  ujumbe wa  ziada  unaliowekwa  katika  sekretariati  ya  Umoja  wa  mataifa , ughali wa maisha  na  marekebisho  ya  kiwango  cha  ubadilishaji fedha, kwa  mujibu  wa  wanadiplomasia.

Bendera katika jengo la Umoja wa Mataifa mjini New YorkPicha: picture-alliance/J. Schwenkenbecher

Hizi ni  pamoja  na  ujumbe  wa  uangalizi  nchini Yemen , ujumbe  wa kisiasa  ulioundwa  nchini  Haiti, uchunguzi wa  uhalifu  wa  kivita uliofanyika  nchini  Syria  tangu  kuzuka  kwa  vita  vya  wenyewe kwa wenyewe  mwaka  2011, na Myanmar  baada  ya  ukandamizaji wa  mwaka  2017 dhidi  ya  waislamu  Warohingya  ambao  ni  jamii ya   wachache  nchini  humo.

Kwa  mara  ya  kwanza , bajeti  kwa  ajili  ya  uchunguzi  nchini  Syria na  Myanmar, ambao hapo awali  ulikuwa  ukigharamiwa  na michango  ya  hiari, katika  mwaka  2020 utahamishiwa  katika  bajeti ya  sekretariati  ya  Umoja wa  mataifa  na  utapatiwa  michango  ya lazima  kutoka  kwa  matifa  wanachama  193.

Urusi  ilipendekeza  mabadiliko  kadhaa  wakati  wa  majadiliano katika  kamati juu  ya mikutano  ya  masuala  ya  bajeti na  kikao cha utendaji  cha  baraza  kuu  la  Umoja  wa  mataifa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia kikao cha ufunguzi cha baraza kuu mnamo seotemba 24 , 2019.Picha: Reuters/B. Mcdermid

Maazimio ya UN

Katika  kila  kura , Urusi, Syria, Myanmar  na  waungaji  mkono  wao, ikiwa  ni  pamoja  na  Korea  kaskazini, Iran, Nicaragua na Venezuela, kulikuwa  na  wingi  mkubwa  dhidi  yao. Wote wamesema  kuwa  wanajitenga na maelezo  ya  mfumo  wa uchunguzi  katika  maazimio  hayo  yaliyoidhinishwa.

Urusi imesema  itachunguza  malipo yake  ya  lazima  ya  hapo baadaye kutokana  na  matokeo  ya  kura na  kutabiri  ongezeko  la malipo  ya  nyuma ambayo  kwa  hivi  sasa  yanakabili  hazina ya Umoja  wa  mataifa  kutokana  na  mataifa  kutolipa  vya  kutosha.

Urusi  imedai  jana  Ijumaa  kuwa  mfumo  wa  uchunguzi  hauna uhalali, wakati Syria  imesisitiza  kuwa  haina mamlaka  kutoka baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  mataifa.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio GuterresPicha: Reuters/C. Allegri

Bajeti  ya  matumizi  ya  Umoja  wa  mataifa  ni  tofauti  kutoka  bajeti ya  mwaka  kwa  ajili  ya  operesheni  za  kulinda  amani  ya kiasi cha  dola  bilioni 6 ambazo ziliidhinishwa  mwezi  Juni.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW