1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNEA yakutana Nairobi kujadili ushirikiano dhidi ya migogoro

26 Februari 2024

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA) linafanya mkutano wake jijini Nairobi kujadili jinsi mataifa yanavyoweza kushirikiana kukabiliana na migogoro kama vile mabadiliko ya tabianchi na kupotea kwa viumbe hai.

Mkuu wa Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, Inger Andersen (kushoto), akiwa na mawaziri wa mazingira wa Sweden na Kenya.
Mkuu wa Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, Inger Andersen (kushoto), akiwa na mawaziri wa mazingira wa Sweden na Kenya.Picha: Jessica Gow/TT NEWS AGENCY/REUTERS

Kabla ya mkutano huo, Mkuu wa Mpango wa Kimataifa wa Mazingira (UNEP), Inger Andersen, ameliambia shirika la habari la AP kwamba hakuna binaadamu yeyote anayeishi peke yake na kwamba kila mtu anaishi katika sayari ya dunia.

"Kila mmoja lazima ashirikishweo kwa kuwa njia ya pekee ya kutatua baadhi ya matatizo hayo ni kwa mazungumzo ya pamoja." Alisema.

Athari za mvua Dar es Salaam

01:02

This browser does not support the video element.

Mkutano huo katika mji mkuu wa Kenya ni kikao cha sita cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kinachohudhuriwa na nchi wanachama, mashirika ya kiraia, wanasayansi na sekta binafsi.

Katika mkutano huo, nchi wanachama hujadili rasimu za maazimio kuhusu masuala mbalimbali ambayo baraza hilo hupitisha baada ya makubaliano.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW