1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNGA: Viongozi wahimiza upatikanaji wa suluhu ya mizozo

27 Septemba 2024

Mkutano wa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa unaendelea mjini NewYork, huku wakuu wa nchi na serikali wakiendelea na juhudi za kutafuta suluhu za changamoto za kimataifa ikiwemo mizozo.

Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa
Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa Picha: Bianca Otero/ZUMA Wire/IMAGO

Katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Kenya William Ruto amesema kufikia Januari mwaka ujao, nchi yake itatuma maafisa zaidi wa polisi nchini Haiti hadi kukamilisha kikosi cha maafisa 2,500.

Ruto ameyasema haya katika mkutano huo; "kufuatia uidhinishaji wa Baraza la Usalama chini ya azimio nambari 2699, Kenya imetuma maafisa wa polisi 382 waliopata mafunzo maalumu nchini Haiti. Siku chache zilizopita, nilipata fursa ya kufanya ziara Haiti, na kushuhudia kazi nzuri ya maafisa wetu nchini humo. Msaada wetu kwa Polisi ya Kitaifa nchini Haiti umesaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha utulivu katika  miji, kulinda miundombinu muhimu na kuleta afueni kwa  jamii nyingi zilizokuwa zimelemazwa na magenge ya wahalifu."Viongozi wawasili kwa ajili ya Mkutano wa Baraza Kuu la UN mjini New York

Ruto alitumia hotuba yake kuomba ufadhili zaidi ili kuunga mkono kikosi hicho cha kupambana na uvunjaji wa sheria ulioenea na kuisaidia nchi hiyo ya Carribean kukabiliana na ghasia za magenge ya wahalifu ambao kwa sasa wanadhibiti asilimia 80 ya mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.

Rais wa Kenya William Ruto akihutubia UNGAPicha: Frank Franklin II/AP Photo/picture alliance

Tukiangazia mzozo wa Sudan, mkuu wa jeshi la nchi hiyo Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan, alipohutubia Mkutano huo Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, amesema wamefanya kila waliwezalo ili kukomesha vita vinavyoendelea na uharibifu unaofanywa na wanamgambo ambao amesema wanazuia juhudi za amani. Al-Burhan amelitolea pia wito baraza hilo kuitambua RSF kama kundi la kigaidi.Zelensky: Urusi inapanga kushambulia mitambo yetu ya nyuklia

Kwa upande wake, Mkuu wa kikosi cha RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, ameliambia baraza hilo kupitia video iliyorekodiwa kwamba kundi hilo liko tayari kutekeleza mpango wa usitishaji vita kote nchini Sudan ili kuruhusu utoaji wa misaada ya kibinadamu.

Kwa upande wake akihutubia mkutano huo wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, ametoa mwito wa kuwa na kiongozi wa kwanza mwanamke kuungoza Umoja huo baada ya takriban miaka 80 ya uongozi wa kiume.

Kwa nini uwakilishi wa Afrika ni muhimu katika Baraza la Usalama ?

02:46

This browser does not support the video element.

Baerbock ameongeza kuwa wanawake wanajumuisha asilimia 50 ya idadi ya watu katika kila nchi lakini kwa muda wa miaka 80 Umoja huo haujawahi kuwa na katibu mkuu mwananmke.

Waziri huyo pia amesema ikiwa shirika hilo linatoa wito wa usawa na haki kote duniani, basi wakati umewadia kudhihirisha hilo ndani ya Umoja huo wa Mataifa. Guterres, atahadharisha juu ya Lebanon kugeuka Gaza nyingine

Kufikia sasa, kumekuwa na makatibu wakuu tisa wa Umoja huo wote wakiwa wanaume ikiwa ni pamoja na wa sasa Antonio Guterres, ambaye muhula wake wa pili uongozini unakamilika mwaka 2026, na ambaye ameelezea kuunga mkono kuweko kwa mrithi mwanamke.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW