1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNHCR:Katika wiki moja wakimbizi milioni waliikimbia Ukraine

3 Machi 2022

Wakimbizi milioni moja wamekimbia Ukraine ikiwa ni wiki moja tangu uvamizi wa Urusi. Umoja wa Mataifa umeonya kuwa kama vita hivyo havitasitishwa mara moja, mamilioni zaidi huenda wakakimbia.

Polen | Ukrainische Flüchtlinge am Grenzübgang Korczowa
Picha: Czarek Sokolowski/AP Photo/picture alliance

Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa - UNHCR Filippo Grandi amesema idadi ya wakimbizi wanaokimbia vita Ukraine inapanda kwa kasi ya ajabu.

Amesema katika miaka yake 40 aliyofanya kazi za kuwashughulikia wakimbizi, hajawahi kushuhudia mmiminiko mkubwa wa wakimbizi kama huo. Zaidi ya nusu ya watu waliokimbia Ukraine wameingia katika nchi jirani ya Poland.

Moldova, Hungary na Slovakia pia zimewakaribisha wakimbizi wengi. Grandi amesema wahudumu wa UNHCR na mashirika mengine wanafanya kazi panapowezekana kuwashughulikia waathiriwa wa vita ndani ya Ukraine chini ya mazingira ya kuogofya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW