1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

UNHCR yahofia kutekelezwa wakimbizi wa Rohingya

17 Oktoba 2023

Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Filipo Grandi, amesema kupungua kwa msaada kwa wakimbizi wa jamii ya Rohingya kunatishia kuchochea mojawapo ya migogoro mikubwa ya kibinaadamu duniani.

Cox's Bazar, Rohingya, Bangladesh
Kambi ya wakimbizi ya Cox Barazaar kwa aili ya wakimbiyiPicha: DW

Grandi amewaambia waandishi habari kandoni mwa mkutano wa kikanda unaofanyika mjini Bangkok, Thailand, kwamba msaada wa kibinaadamu unapunguwa kutokana na mizozo nchini Ethiopia, Sudan, Afghanistan, Ukraine na Israel.

Soma zaidi: Warohingya wakumbuka miaka sita ya mauaji ya halaiki

Amesisitiza kwamba mzozo wa Rohingya haupaswi kusahaulika na kama michango itapungua kutakuwa na shida.

Grandi pia amesema mzozo wa Rohingya ulikuwa na asilimia 42 ya kiwango jumla cha fedha cha milioni 875.9 zinazohitajika mwaka huu.