UNHCR yakosoa sera za Marekani kuhusu wahamiaji
7 Oktoba 2025
Akizungumza mjini Geneva, Grandi ametumia hotuba yake kulalamikia kupunguzwa kwa ufadhili na rasilimali ndani ya shirika hilo, akibainisha kuwa hatua hiyo imesababisha kupotea kwa takriban ajira 5,000 mwaka huu — sawa na karibu robo ya wafanyakazi wake.
Hata hivyo, Grandi amesifu baadhi ya juhudi za utawala wa Trump, hasa zile zinazolenga kuleta amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako mamilioni ya watu wamelazimika kukimbia makaazi yao kutokana na vita.
Katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika mwezi uliopita, serikali ya Trump — ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa misaada ya kibinadamu ya kimataifa mwaka huu — iliwahimiza washirika wake kuunga mkono mtazamo wake kwamba mfumo wa kimataifa wa kuwahifadhi wakimbizi umetumiwa vibaya na unahitaji kufanyiwa marekebisho, ikiwemo udhibiti zaidi wa uhamiaji.