1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNHCR yaomba ufadhili zaidi wakati wakimbizi wakiongezeka

14 Desemba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi UNHCR, limetahadharisha juu ya kuongezeka idadi ya watu waliokimbia makazi yao.

Umoja wa Mataifa I Mkuu wa Shirika la wakimbizi UNHCR Filippo Grandi
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuwahudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi Picha: Fabrice Coffrini/AFP

Shirika hilo limesema linakabiliwa na uhaba wa fedha jambo linalolazimisha kupunguza wafanyakazi katika shirika hilo pamoja na kupunguza shughuli zake.

Akihutubia Kongamano la Kimataifa la Wakimbizi huko Geneva nchini Uswisi hapo jana , mkuu wa UNHCR Filippo Grandi alitoa wito kwa wafadhili kuongeza misaada yao ili kushughulikia idadi inayoongezeka ya watu wanaolazimika kuyahama makazi yao kutokana na migogoro na mabadiliko ya tabianchi.

Soma pia:UN: Watu 450,000 wameyakimbia mapigano mashariki mwa DRC

Grandi amesema Mashirika mengi ya kibinadamu yanakabiliwa na changamoto kubwa za ufadhili na kwamba UNHCR pekee imepungukiwa kiasi cha dola milioni 400 za kuweza kukidhi mahitaji hadi mwishoni mwa mwaka.

Grandi amevitaja vita katika Ukanda waGaza, Ukraine na Sudan kuwa vimesababisha matumizi makubwa na huduma zake ambapo shirika hilo limelazimika kuahirisha au kupunguza baadhi ya shughuli zake katika maeneo mengine.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW