1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Watoto 1,000 wanakufa kila siku kwa kunywa maji machafu

20 Machi 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto, UNICEF, limesema kukosekana kwa miundombinu ya usafi na unywaji wa maji machafu kunahatarisha maisha ya watoto kote ulimwenguni.

Afrika Cholera Nigeria
Picha: Gilbertson/Zumapress/picture alliance

Taarifa iliyotolewa leo na UNICEF, imeeleza kuwa kila siku zaidi ya watoto 1,000 wenye chini ya umri wa miaka mitano wanakufa duniani kote kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu na mazingira machafu.

Soma pia:UNICEF: Mamilioni hawana maji safi Pembe ya Afrika 

Kulingana na utafiti mpya wa UNICEF, jumla ya watoto milioni 190 kwenye nchi 10 za Afrika wako hatarini. Hali ni mbaya zaidi kwenye nchi za Benin, Burkina Faso, Cameroon, Chad, Ivory Coast, Guinea, Mali, Niger, Nigeria na Somalia.

Jumatano ni Siku ya Maji Duniani. Pia ni siku ya kuanza kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW