1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF: Watoto Kongo wakabiliwa na hatari ya unyanyasaji

30 Desemba 2025

Watoto nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanakabiliwa na hatari ya kukumbwa na vitendo vya unyanyasaji wa kingono ambavyo vinasalia kuwa mgogoro ulioenea na unaovuruga utulivu.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Watoto wanajeshi nchini KongoPicha: Zanem Nety Zaidi/DW

Hayo yameelezwa leo katika ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto (UNICEF), ripoti iliyoongeza kuwa miaka thelathini ya mzozo mashariki mwa Kongo ni moja ya sababu kubwa ya madhila hayo kwa watoto yanayochagizwa na mifumo dhaifu ya ulinzi na uwajibikaji mdogo wa kisheria.

Lakini pia UNICEF imeripoti vitendo vya unyanyasaji mkubwa wa kingono hata nje ya maeneo yenye migogoro na kwamba licha ya miongo kadhaa ya juhudi endelevu za kitaifa na kimataifa, ukiukwaji huo unaendelea katika viwango vya kutisha kote nchini Kongo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW