1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiYemen

UNICEF: Watoto milioni 11 wanategemea misaada ya kiutu Yemen

24 Machi 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto, UNICEF limesema maisha ya watoto milioni 11 nchini Yemen yanategemea misaada ya kiutu.

Jemen Hilfe Katastrophenhilfe Flüchtlinge Flucht
Picha: ESSA AHMED/AFP/Getty Images

UNICEF aidha limeonya mapema leo kwamba wasichana milioni 2.2 pamoja na wavulana wanaugua utapiamlo na bila ya hatua za dharura, kitisho kitakuwa kikubwa zaidi.

Zaidi ya watoto 540,000 wanakabiliwa na utapiamlo mkali unachotishia maisha yao iwapo hawatapata tiba ya haraka, limesema shirika hilo.

Soma pia: Umoja wa Mataifa wakusanya dola bilioni 1.2 kuisaidia Yemen

Yemen kwa muda mrefu imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya upande unaoongozwa na Saudi Arabia na wanamgambo wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran na kufanya hali ya kiutu nchini humo kuwa mbaya.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW