Mabadiliko ya tabianchi yawahamisha Watoto milioni 43.1
6 Oktoba 2023Matangazo
Shirika hilo limeuonya kuwa huu ni mwanzo tu na kusema hayo yinachochewa na ongezeko la joto duniani, ambapo sehemu zilizokumbwa zaidi na kadhia hiyo ni Ufilipino, India, China, Canada na Marekani.
Makadirio ya muda yanaonesha kuwa mafuriko yanayohusishwa na mito kuvunja kingo zake, yanaweza kupelekea watoto milioni 96 kuyahama makazi yao katika miaka 30 ijayo. Vimbunga vinakadiriwa kuwa vitawahamisha watoto milioni 10.3 huku dhoruba ikiwahamisha milioni 7.2.