1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

UNICEF yalaani ongezeko la ukatili dhidi ya watoto, Sahel

30 Mei 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF, limelaani ongezeko la asilimia 70 la unyanyasaji mkubwa dhidi ya watoto nchini Mali, Burkina Faso na Niger

Wanajeshi wa Burkina Faso washika doria kwenye barabara ya Gorgadji katika eneo la Sahel mnamo Machi 3, 2019
Wanajeshi wa Burkina Faso washika doria kwenye barabara ya Gorgadji katika eneo la SahelPicha: LUC GNAGO/Reuters

Gilles Fagninou, mkurugenzi wa UNICEF katika kanda ya Afrika Magharibi na Kati, amesema katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2023, ukiukwaji mkubwa dhidi ya watoto katika eneo la kati la Sahel, uliongezeka kwa zaidi ya asilimia 70 ikilinganishwa na miezi mitatu ya awali.

Watoto walitumiwa kufanya mauaji

Fagninou ameongeza kuwa visa vingi vilihusisha kusajiliwa na kutumiwa kwa watoto katika makundi yenye silaha pamoja na kufanya mauaji.

Soma pia:Watoto milioni 1.8 wamekimbia makaazi yao ukanda wa Sahel

Afisa huyo wa UNICEF pia amesema ongezeko la kusikitisha la matukio ya kikatili katika eneo la kati la Sahel lazima likomeshwe ikiwa watoto watahitajika kutambua haki zao za kimsingi za maisha.