1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF yaionya Afrika dhidi ya kufunga skuli kwa corona

Deo Kaji Makomba
22 Septemba 2020

Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limezionya nchi za mashariki na kusini mwa Afrika kuwa ziko katika hatari ya kupoteza kizazi ikiwa hazitofunguwa skuli kwa ajili ya masomo kufuatia mripuko wa COVID-19.

Symbolbilder | Laut UNICEF können Hunderte Millionen Kinder in Schulen nicht Händewaschen
Picha: picture-alliance/dpa/XinHua/S. Zounyekpe

Bodi ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa imesema licha ya baadhi ya nchi kufungua skuli kwa ajili ya kuanza tena masomo, karibu watoto milioni 65 wako nje bila kuendelea na masomo yao.

Mataifa mengine, kama vile Kenya, hayana uhakika ikiwa skuli zao zitafunguliwa tena mwaka huu ama la.

Miezi saba ndani ya mripuko wa janga hilo ni lazima tuwe wazi kabisa juu ya ukubwa wa tatizo hili. Tupo katika hatari ya kupoteza kizazi," alisema Mohamed Malick Fall, mkurugenzi wa UNICEF katika eneo la mashariki na kusini mwa Afrika.

"Tunashuhudia kupotea fursa ya kupata elimu, kuongezeka kwa ukatili, kuongezeka kwa ajira kwa watoto, ndoa za utotoni, mimba za utotoni na kupungua kwa lishe. Kizazi cha watoto kiko katika hatari na huu ni wakati muhimu zaidi katika historia ya bara letu," aliongeza mkurugenzi huyo.

Aidha UNICEF imesema kuwa mamilioni ya watoto wanakosa lishe bora kutokana na kuwa nje ya skuli.

Skuli zinaweza kufunguliwa salama licha ya janga linaloendelea, kwa mujibu wa timu ya wataalamu wa Shirika jilo, ambayo ilibainisha kuwa ushahidi wa kisayansi unaonesha kuwa watoto sio waenezaji bora wa virusi vya corona, licha ya kuwa wao ndio walioathiriwa pakubwa kwenye juhudi za kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo katika ukanda huo.

"Sasa tunajua hatari kubwa kwa watoto kuwa nje ya madarasa," ilisema taarifa hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW