1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF yasaka dola bilioni 9.9 kwa watoto maeneo ya vita

5 Desemba 2024

Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetangaza kampeni ya kusaka dola bilioni 9.9 kwa ajili ya misaada kwa mamilioni ya watoto walioathirika kwa vita na mizozo mingine ulimwenguni.

Gaza, polio, UNICEF
Wahudumu wa UNICEF wakigawa chanjo za polio kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: Hani Alshaer/Anadolu/picture alliance

Mkurugenzi mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell, amesema kwenye taarifa yake ya leo kwamba kiwango cha watoto wanaoteseka na wenye mahitaji kimefikia hali ambayo haijawahi kutokea kwenye historia ya ulimwengu, na kwamba wengine wengi wanaendelea kuathirika kila siku.

Fedha hizo zitaelekezwa kwa watoto milioni 109 na kusaidia kwenye miundombinu ya kimsingi ya afya, huduma za afya ya akili, maji na elimu, lishe na mapambano dhidi ya dhuluma za kijinsia.

Soma zaidi: UNICEF: Mamilioni ya wasichana wadhalilishwa kingono

Sehemu kubwa ya fedha hizo ni kwa ajili ya Afghanistan, Sudan, Kongo, Palestina na Lebanon.

Kampeni hii ya UNICEF inatangazwa wakati operesheni za misaada ya kibinaadamu zikikumbwa na uhaba mkubwa wa fedha kote ulimwenguni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW