1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Union Berlin yamtimua kocha Nenad Bjelica

6 Mei 2024

Klabu inayokabiliwa na shoka la kushuka daraja Union Berlin imemtinua kocha wake Nenad Bjelica Jumatatu, siku moja baada ya rais wa klabu hiyo ya Bundesliga kumuunga mkono raia huyo wa Croatia.

Kocha wa Union Berli aliyetimuliwa Nenad Bjelica
Kocha wa Union Berli aliyetimuliwa Nenad BjelicaPicha: BEAUTIFUL SPORTS/Meusel/picture alliance

Union Berlin walipoteza 3-4 dhidi ya mahasimu wanaokabiliwa na kitisho cha kushuka daraja Bochum Jumapili na wamesimama nafasi moja tu kutoka eneo la kucheza mechi za mchujo huku zikisalia mechi mbili kabla msimu kukamilika.

Bjelica alichukua mikoba kuikufunzi Union Novemba mwaka uliopita baada ya kocha wa wakati huo Urs Fuíscher kufutwa kazi kufuatia matokeo mabaya licha ya kuiwezesha timu hiyo kufuzu kwa kombe la mabingwa Ulaya, Champions, kwa mara ya kwanza msimu uliotangulia.

Taarifa ya klabu imesema Marco Grote, pamoja na kocha msaidizi, Marie-Louise Eta, wataisimamia timu hiyo kwa mechi mbili zilizosalia, likiwemo pambano kali la kujaribu kuepuka shoka la kushuka daraja dhidi ya Cologne.

Grote aliwahi kuisimamia Union Berlin katika kipindi cha kati ya kocha Fischer na Bjelica. "Katika mapambano ya kuendelea kucheza Bundesliga tunahitaji kuonesha nguvu za klabu yetu yote. Tunamuamini Marco Grote na timu yake kuwaongoza wachezaji katika viwango vyao bora," alisema rais wa Union, Dirk Zingler, katika taarifa.

Soma pia: Bundesliga yashuhudia mvua ya magoli

Siku ya Jumapili, kabla kupoteza pambano dhidi ya Bochum, Zingler aliimbia DZAN: "Nenad Bjelica ana uungwaji mkono wetu kamili." Kauli hii ilifuatia ripoti za vyombo vya habari zilizosema mabadiliko ya kocha yangefanyika.

Bjelica alichukua mikoba kutoka kwa Urs Fischer

Bjelica alikuwa chaguo la kushutukiza kuchukua nafasi ya kocha maarufu Urs Fischer ikizingatiwa mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Kaiserslautern hakuwa na uzoefu wowote wa ukocha nchini Ujerumani wala nje ya nchi yake alikozaliwa ya Croatia katika ngazi ya juu.

Chini ya kocha Bjelica, Union mwanzoni iliimarika lakini raia huyo wa Croatia alisababisha gumzo kubwa mnamo Januari alipomvuruta uso kiungo wa Bayern Munich, Leroy Sane, na akafungiwa mechi tatu. Vyombo vya habari viliripoti kwamba Union ilikaribia kumtimua wakati huo lakini sasa wameamua kuchukua hatua huku matokeo yakiendelea kuwa mabaya.

"Ningependa kumshukuru Nenad Bjelica na timu yake kwa kazi waliyoifanya," Zingler aliongeza kusema katika taarifa. "Walifanikiwa kuiimrisha timu katika hali ngumu, kwa matokeo kwamba kuwa juu kuko mikononi mwetu."

Cologne, ambayo iko katika nafasi mbili za mwisho za kushuka daraja moja kwa moja, iko alama sita nyuma ya Union Berlin na lazima ishinde mechi yao ya Jumamosi kujihakikishia nafasi ya kuendelea kucheza Bundesliga.

Union Berlin, ambao wamecheza misimu mitano katika Bundesliga, wanapambana na Mainz, inayoshikilia nafasi ya kucheza mechi za mchujo lakini iliyo katika fomu nzuri.

(dpae)