United kidedea, Arsenal hoi
30 Novemba 2020Matangazo
Arsenal walikuwa nyumbani Emirates wakiwaalika Wolverhampton Wanderers na wakabebeshwa magoli mawili kwa moja katika mechi ambayo mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez alipata jeraha baya la kichwa alipogongwa na beki wa Arsenal David Luiz walipokuwa wakiwania mpira wa kona. Ripoti zinaarifu kwamba kwa sasa Jimenez anaendelea vyema ingawa bado yuko hospitali.
Dabi ya London kati ya Tottenham Hotspur na Chelsea iliyompatanisha kocha na mwanafunzi wake, Jose Mourinho na Frank Lampard, iliishia sare ya kutofungana.