United yajiandaa kupambania taji la EPL
21 Agosti 2026
United ilimaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita chini ya Carrick, baada ya kuteuliwa kuwa kocha wa muda kufuatia kuondoka kwa Ruben Amorim, na mashabiki wana matumaini ya kutwaa taji lao la kwanza tangu 2013.
Carrick, ambaye sasa ni kocha wa kudumu, anasema klabu "inafanya kazi kuimarisha kikosi” kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa Septemba 1. Tayari United imewasajili Youri Tielemans, Andrey Santos na kipa Karl Darlow.
United pia inawinda beki wa kushoto, lakini Carrick anasisitiza timu lazima ijiandae vizuri kwa mechi za kwanza dhidi ya Hull na Ipswich, akisema hakuna mechi rahisi dhidi ya timu zilizopandishwa daraja.
Wakati huo huo kiungo wa kati Mason Mount amerudi mazoezini lakini jeraha dogo linaweza kumkosesha mchezo wa Jumamosi, huku Carrick akisema "ni kitu kidogo, hakuna taharuki."