AfyaMarekani
Wataalamu wa upasuaji wapandikiza jicho kwa mara ya kwanza
10 Novemba 2023Matangazo
Pamoja na mafanikio hayo bado haiko wazi iwapo mtu aliyepandikizwa jicho hilo ataweza kuona tena.
Upasuaji huo wa kwanza ulihusisha kuondoa sehemu ya uso na jicho zima la kushoto ikijumuisha mishipa ya kusambaza damu na mishipa ya macho ya mfadhili wa jicho hilo na kupachika kwa mgonjwa.
Mgonjwa huyo Aaron James alipata majeraha makubwa ya jicho baada ya kupigwa na shoti ya umeme, Juni 2021 ikiwa ni pamoja na kupoteza jicho la kushoto na viungo vingine.
Madaktari wamekuwa wakifanya majaribio ya upasuaji kama huo kwa wanyama na kuwarejeshea uoni kiasi, lakini hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa binaadamu.