1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya uhusiano wa Israel na Saudi Arabia kukamilika

23 Septemba 2023

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema makubaliano ya kurejesha mahusiano kati ya nchi yake na Ufalme wa Saudi Arabia yako njiani kukamilika.

USA | UN Generalversammlung in New York | Benjamin Netanjahu
Picha: Richard Drew/AP Photo/picture alliance

Akizungumza na kituo cha televisheni ya Fox News cha nchini Marekani usiku wa kuamkia leo, Netanyahu alisema ni vyema makubaliano hayo yakahitimishwa ndani ya kipindi cha miezi michache ijayo. Kwa miezi kadhaa sasa, kumekuwa na uvumi ikiwa Saudi Arabia inaweza kuwa nchi nyengine ya Kiarabu kurejesha uhusiano wake na Israel, lakini mara kadhaa pande husika zilikuwa haziweki bayana jambo hilo. Mnamo Septemba mwaka 2020, Muungano wa Falme za Kiarabu na Bahrain zilikuwa nchi za kwanza za Ghuba kuanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Israel kupitia makubaliano yaliyosimamiwa na serikali ya Marekani.  Ingawa Saudia haina uhusiano wowote na Israel, mataifa hayo mawili yamekuwa yakishirikiana kwenye masuala ya usalama kwa miaka kadhaa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW