Upigaji kura waanza nchini Uganda katika uchaguzi wa rais
15 Januari 2026
Umati mkubwa wa watu umejitokeza na foleni ndefu kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo huku vituo vya kupigia kura vikichelewa kufunguliwa .
Mmoja wa wapiga kura nchini humo Najjemba Jamidah ameelezea hali iliyoshuhudiwa katika vituo hivyo saa za asubuhi.
''Kweli, nilikuja hapa karibu saa moja na nusu asubuhi kwasababu walituambia kufikia saa moja shughuli ya kupiga kura itaanza. Lakini bado tuko hapa tumesimama, tukingojea mashine. Wanatuambia mashine bado hazijafika. Kwa hivyo tunasubiri tu na tunatumai tutapiga kura kwa wakati."
Wakati huo huo, katibu mkuu wa chama cha upinzani cha National Unity Platform, David Lewis Rubongoya, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kucheleweshwa kwa zoezi hilo ni hatua ya makusudi na kuongeza kuwa hakukuwa na matatizo katika maeneo walikopiga kura wanajeshi.