Upigaji kura wafanyika kwa amani Nepal baada ya mapinduzi
5 Machi 2026
Matangazo
Maafisa wa usalama wamepiga doria na kuvilinda vituo vya kupigiakura katika taifa hilo lililoko katika milima ya Himalaya, huku wapiga kura wakipanga mistari kupiga kura zao.
Kulingana na maafisa, kampeni zilifanyika kwa amani kuelekea Alhamis ya leo ya upigaji kura. Mamlaka zimepiga uendeshaji wa magari barabarani pamoja na kufanyika mikutano ya kisiasa.
Kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo, yapata watu milioni 19 kati ya idadi jumla ya watu milioni 30 nchini humo wamejiandikisha kupiga kura.
Karibu Wanepal milioni 3 wanaishi nje ya nchi ila hawatoweza kushiriki upigaji kura.